array(0) { } Radio Maisha | Raila ayapongeza mataifa ya afrika kwa juhudi za kukabili korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Raila ayapongeza mataifa ya afrika kwa juhudi za kukabili korona

Raila ayapongeza mataifa ya afrika kwa juhudi za kukabili korona

Mjumbe Maalumu wa Ujenzi na Muundo Msingi Barani Afrika Raila Odinga ameyaopongeza mataifa ya Afriika jinsi yamejizatiti katika kukabili Korona.

Akihojiwa na Runinga ya SABC, Raila amesema mikakati iliyowekwa na mataifa ya Kenya, Afrika Kusini, Uganda, Naijeria miongoni mwa mengine, imesaidia pakubwa katika kukabili Korona,  ikizingatiwa kwamba Afrika ni Bara lenye mataifa yenye watu wengi maskini.

Raila amesema licha ya mataifa haya kukosa vifaa muhimu vya kudhibiti Korona, juhudi zilizoowekwa na viongozi wake zimewalinda raia.

Kuhusu athari ya Korona kwenye uchumi wa mataifa mengi Duniani, Raila ambaye pia ni Kinara wa ODM amesema viongozi wa Afrika wana jukumu kuu la kufufua uchumi baada ya biashara nyingi kusimama wakati wa Korona.

Ameeleza haja ya wajasiriamali kuwekeza zaidi katika sekta mbalimbali ili kufufua uchumi punde tu virusi hivyo vitakapodhibitiwa.

Raila amesisitiza kwamba ni wakati wa Waafrika kutathmini utayarifu wao katika kukabili majanga mbalimbali yakiwamo magonjwa, huku akihimiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kushirikiana kwenye utafiti na ubunifu wa kiteknolojia ili kujitegemea.