array(0) { } Radio Maisha | Idara ya mahakama imepewa tarakilishi 40 kufanikisha kusikilizwa kwa kesi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Idara ya mahakama imepewa tarakilishi 40 kufanikisha kusikilizwa kwa kesi

Idara ya mahakama imepewa tarakilishi 40 kufanikisha kusikilizwa kwa kesi

Muungano wa Bara Uropa umepiga jeki mikakati ya kukabili janga korona katika Idara ya Mahakama humu nchini.

Muungano huo umetoa takribani tarakilishi arubaini za kurahisisha matumizi ya kidijitali katika idara hiyo wakati huu wa janga hilo.

Tarakilishi hizo thelathini zimetolewa kwa awamu ya kwanza huku zikitarajiwa kufanikisha kusikilizwa kwa kesi mbalimbali kupitia njia ya kidijitali.

Jaji Mkuu David Maraga amesema matumizi ya kidijitali ndiyo suluhu ya pekee kwa Idara hiyo katika kuzuia maambukizi ya Korona na kupunguza mirundiko ya kesi mahakamani.

Balozi wa Uropa humu nchini amesema matumizi ya teknolojia yatawawezesha wataalamu wanaofuatilia kesi mbalimbali kutopoteza wakati mwingi, na hivyo kuboresha utendakazi wa mahakama na haki kwa wanaodhulumiwa.