array(0) { } Radio Maisha | Serikali imetangaza marufuku ya kutoka na kuingia Eastleigh,Nairobi na Old Town Mombasa, huku maambukizi ya korona yakiongezeka
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali imetangaza marufuku ya kutoka na kuingia Eastleigh,Nairobi na Old Town Mombasa, huku maambukizi ya korona yakiongezeka

Serikali imetangaza marufuku ya kutoka na kuingia Eastleigh,Nairobi na Old Town Mombasa, huku maambukizi ya korona yakiongezeka

Kuanzia leo hii dakika chache zilizopita hakuna kutoka wala kuingia mtaani Eastligh Nairobi na Old Told Town Jijini Mombasa. Serikali imetangaza marufuku hayo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya korona.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe aidha amesema masoko yote, hoteli na mikahawa itasalia kufungwa kwa muda huo wa siku kumi na tano.

Waziri Kagwe amewahakikishia wakazi wa maeneo yaliyoathirika kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya Korona nchini, akisema serikali ianendelea kufuatia kwa karibu maeneo mengine ambayo huenda yameathirika zaidi na virusi hivyo akisema maagizo zaidi yatatolewa iwapo kutakuwa na haja.

Hayo yanajiri huku Maambukizi nchini yakifikia mia tano themanini na moja baada ya watu arubaini na saba kuthibitishwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwa waliaombukizwa, thelathini na wawili ni wa mjini Mombasa na kumi na mmoja wakiwa wa Nairobi, huku visa viwili vikiripotiwa Kiambu na Busia, na kisa kimoja kikiripotiwa Kwale.

Imebainika kwamba asilimia tisini ya waliopatikana kwua na korona miongoni mwa arubaini na saba hao hawakuwa na dalili huku waliokuwa na dalili wakiwa asilimia kumi pekee. Daktari Patrick Amoth ni Kaimu Mkurugenzi wa  Matibabu katika Wizara ya Afya.

Watu wawili zaidi wamefariki dunia , hivyo kufikisha idadi jumla kuwa ishirini na sita kote nchini.

Wawili hao walifariki wakiwa nyumbani jijini Mombasa hali ambayo imeibua wasiwasi, kwani huenda kuna watu zaidi ambao wameaambukizwa.

Vilevile, watu wanane zaidi wamethibitishwa kupona na kufikisha mia moja tisini jumla ya watu ambao wamepona nchini.