array(0) { } Radio Maisha | UKATILI WA SERIKALI WADHIHIRIKA WAZI KARIOBANGI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

UKATILI WA SERIKALI WADHIHIRIKA WAZI KARIOBANGI

UKATILI WA SERIKALI WADHIHIRIKA WAZI KARIOBANGI

Zaidi ya familia elfu tano zilizokuwa zikiishi katika ardhi inayoidaiwa kuwa ya serikali katika Mtaa wa Kariobangi Kaskazini zimekesha kwenye baridi. Watu na familia zao hawajui wa kumkimbilia baada ya iliyotarajiwa kuwa ngome yao ya ulinzi yaani serikali kuwa ndiyo yenye kuwadhulumu kupitia maafisa waliofaa kuwalinda na matrekta yaliyofaa kuwajengea mazingira bora zaidi ya kuishi.

Serikali ilichukua hatua hiyo hata pasi na kuzingatia agizo la mahakama la kuzuia kubomolewa kwa makazi ya wanachama hoa wa kikundi cha Kariobangi Sewerage Farmers lililotolewa na Jaji Samson  Okong'o kupitia kesi iliyowasilishwa na wakili John Khaminwa.

Cha kuhuzunisha ni kwamba serikali imechukua hatua hiyo wakati ambapo dunia nzima ina mahangaiko tele yasiyomsaza mdogo wale mkubwa. Hivi sasa kuanzia wakongwe hadi watoto wenye umri wa miezi tu na wengine  siku kadhaa hawajui waende wapi. Baadhi wangetamani kwenda mashinani lakini hilo pia haliwezekani kufuatia marufuku ya usafiri. Pia wangetamani kufadhiliwa angalau na hema na chakula lakini ao hao waliotarajia kuwapa ndio wamewafurusha.

Serikali imejaa watu ambao walilelewa mazingira sawa na hayo na hata mabaya  zaidi na  bila shaka yoyote wanaelewa fika kufika kuna maisha ambayo si ya kuchagua. Maisha ya uskwota na mabanda si ya kuchagua ni ya kujipata na kupambana nayo na kutia dua kwamba 'Ipo siku yataisha'.

Mbona basi serikali inayochukua kodi kutoka kwa wananachi ao hao ipuuze haki zao, kwanza kwa kukiuka mahakama lakini zaidi kwa kuwachukulia kuwa viumbe hayawani. Hapa Radio Maisha tunaikumbusha serikali kwamba mamlaka iliyonayo imekabidhiwa na wananchi wenyewe kupitia katiba. Kipengee cha kwanza, sehemu ya kwanza kinasema  kwa kiingereza.
 

1.Sovereignty of the people
(1)All sovereign power belongs to the people of Kenya and shall be exercised only in accordance with this Constitution.

 
Hili lisiwahi kusahaulika kamwe.