array(0) { } Radio Maisha | Rais Farmajo afanya mazungumzo ya simu na rais Kenyatta
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Farmajo afanya mazungumzo ya simu na rais Kenyatta

Rais Farmajo afanya mazungumzo ya simu na rais Kenyatta

Rais wa Somalia Mohamed Farmajo amempigia simu Rais Uhuru Kenyatta na kumpa rambirambi kufuatia vifo vya marubani wawili wa Kenya walioangamia kufuatia ajali ya ndege nchini humo.

Farmajo ameiomba Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini kushirikiana na wenzao wa Somalia kuchunguza utata unaozingira kuanguka kwa Ndege ya African Airline, katika eneo la Bardale nchini Somalia.

Mazungumzo hayo yamejiri saa chache tu baada ya Kenya kushinikiza uchunguzi wa kina kufanywa ili kubaini iwapo kundi gaidi la Alshabaab lilihusika au la.

Aidha, tayari Wizara ya Mashauri za Nchi za Kigeni imetoa wito kwa ndege nyingine za Kenya kuwa makini kufuatia tukio hilo.

Ndege hiyo ilianguka na kusababisha vifo vya marubani hao wa Kenya na abiria wanne, baada ya kudaiwa kulipuliwa na kombora. Ndege hiyo ilikuwa ikisafirisha misaada vikiwamo vifaa vya matibabu ili kusaidia katika kukabili janga la korona

Ndege hiyo inayomilikiwa na Shirika la humu nchini la African Express, ilianguka dakika tatu pekee kabla ya kutua.

Shughuli za kuwatambua abiria wawili bado zinaendelea, huku Waziri wa Uchukuzi wa Somalia, Hassan Hussein Mohamed akisema miongoni mwa abiria wanne wawili ni Wasomali..

Kufikia sasa, Mohamed amethibitisha kupatikana kwa mili mitano.