array(0) { } Radio Maisha | Serikali imetangaza jinsi elimu itarejelewa nchini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali imetangaza jinsi elimu itarejelewa nchini

Serikali imetangaza jinsi elimu itarejelewa nchini

Mapumziko ya katikati ya muhula wa pili yatapunguzwa kwa siku nne, huku muhula wa tatu ukipunguzwa kwa wiki mbili ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kusoma zaidi baada ya kuwa nyumbani katika likizo ndefu kufuatia janga la korona.

Haya yanajiri baada ya serikali kutangaza mikakati itakayowekwa katika kuongeza wakati wa masomo, kwenye muhula wa pili na wa tatu kufuatia muda mwingi wa mafunzo uliopotezwa wakati wa kukabili Janga la Korona.

Vilveile, muda wa vipindi vya masomo vitaongezwa kila siku ili kufanikisha kukamilika kwa silabasi kabla ya kufanya mitihani ya Kitaifa KCPE na KCSE.

Kwa mujibu wa stakabadhi ya majibu ya Waziri wa Elimu Prof. George Magoha kwa kamati ya Elimu katika Bunge la Kitaifa, magoha amedokeza uwezekano wa shule kufunguliwa mwezi ujao japo chini ya masharti makali ya kuzuia maambukizi ya Korona.

Magoha alitakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo, ili kueleza jinsi serikali inavyojipanga kubadilisha tarehe za kalenda ya masomo ili kufidia wakati uliopotezwa kwa wanafunzi wakati wa Janga la Korona.

Mara si moja Magoha amekuwa akiwasisitizia wazazi kwamba tarehe za mitihani hazitahairishwa, kwa msimamo kwamba Taasisi ya Kukuza Mitalaa KICD inaendeleza masomo kwa njia ya mitandaoni na vyombo vya habari kama Edu Channel.

Ikumbukwe tarehe kumi na tano mwezi Machi Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kufungwa kwa shule zote na vyuo vikuu baada ya kisa cha kwanza cha Korona kuripotiwa nchini.