array(0) { } Radio Maisha | Kenya yarekodi visa 45 vya korona idadi kubwa zaidi ya maambukizi kwa siku
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kenya yarekodi visa 45 vya korona idadi kubwa zaidi ya maambukizi kwa siku

Kenya yarekodi visa 45 vya korona idadi kubwa zaidi ya maambukizi kwa siku

Kwa mara ya kwanza kabisa tangu kuthibitishwa kwa maambukizi ya virusi vya korona nchini, Kenya imerekodi idadi kubwa zaidi kuwahi kutangazwa tangu Machi 12.

Kufikia sasa Kenya ina visa mia tano thelathini na vitano, baada ya watu wengine arubaini na watano kuthibitishwa kuambukizwa.Chini ya kipindi cha saa ishirini na nne sambuli 177 zimepimwa.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kuhusu takwimu za maambukizi, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba miongozi mwa waliombukizwa 29 ni wa Nairobi, 11 wa Mombasa na watano wa Wajiri huku mmoja akiwa raia wa Somalia. Waathiriwa wa Wajiri wanahistoria ya kusafiri mjini Mogadishu.

Kagwe aidha amesema kuwa miongoni mwa walioambukiwa thelathini ni wanawake huku wanaume wakiwa kumi na watano. Aidha watu 9 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona inchini kuwa 182

Haya yanajiri huku Wizara ya Afya imeonya kuhusu ongezeko la visa vya maambukizi ya ndani kwa ndani kwenye Mitaa ya Eastleigh Kawangware, jijini Nairobi na Old Town mjini Mombasa.

Idadi ya maambukizi mtaani Eastleigh imefikia watu sitini na watatu baada ya watu ishirini na tisa kuthibitishwa leo kuambukizwa korona, Kawangware ikiwa na visa ishirini na vinne huku mtaa wa Old Town ukiwa na visa thelathini na tisa.

Kagwe amesema idadi hiyo imeongezeka kutokana na mpango wa kuwapima watu kwa halaiki Mass Testing ambao unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri , Kagwe aidha ameonya kuhusu unyanyapaa dhidi ya waliopona akihimiza kila mmoja kuwakubali waliopona kuwa sehemu ya jamii.

Aidha Waziri amewashtumu wanaopuuza maagizo ya serikali ukiwamo mwongozo uliotolewa kwa wamiliki wa mikahawa na hoteli kuzingatia kabla ya kurejelea shughuli zao.

Kagwe amesema ni mapema sana kuanza kuendesha shughuli kama kawaida kwani bado visa vya maambukizi vinaongezeka.

Wakati uo huo, Waziri amesema iwapo Wakenya hawatazingatia maagizo yanayotolewa na serikali, basi huenda maambukizi yakaongezaka zaidi na kuilazimu serikali kuongeza masharti makali hasa kwenye maeneo yanaoendelea kuathirika na virusi hivyo.