array(0) { } Radio Maisha | Serikali yatishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia Old Town, Mombasa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali yatishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia Old Town, Mombasa

Serikali yatishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia Old Town, Mombasa

Huenda marufuku ya kutoka na kuingia kwenye eneo la Old Town Kaunti ya Mombasa ikawekwa iwapo wakazi wataendelea kususia mpango wa kuwapima kubaini iwapo wameambukizwa virusi vya korona au la. Kamati iliyobuniwa Kukabili janga la korona katika Kaunti ya Mombasa imetishia kutangaza marufuku hayo kwani kwa siku tatu ambapo shughuli hiyo imeendelea ni watu wachache tu ambao wamejitokeza kupimwa.

Gavana wa Mombasa  Ali Hassan Joho Hassan abaye anaiongoza kamati hiyo, amesema ni jambo la kusikitisha kuona kwamba licha ya eneo hilo kufanywa kipaumbele wakazi wamekuwa wakisusia kupimwa.

Joho amesema tangu shughuli ya kuwapima wakazi wa eneo hilo ilipoanza, ni watu mia moja na thelathini pekee wamepimwa licha ya idadi ya wakazi hao kuwa takriban watu elfu ishirini na nane.

Kauli ya Joho imesisitizwa na Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo.

Gavana Joho aidha amegadhabishwa na hatua ya baadhi ya misikiti kufunguliwa kisiri kuendeleza ibada wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Vilevile amekerwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikashifu juhudi na mikakati ambayo imewekwa katika kaunti hiyo kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir ameapa kuhakikisha kwamba viongozi wa dini wanaoendelea kukiuka maagizo ya serikali wanakamatwa na kushtakiwa.


Kufikia sasa jumla ya watu sita wa eneo la Old Town ni miongoni mwa watu kumi na wawili wa  Kaunti hiyo ya Mombasa waliofariki dunia kufuatia korona.