array(0) { } Radio Maisha | Kenya yarekodi visa 24 vya COVID-19 idadi imefikia 435
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kenya yarekodi visa 24 vya COVID-19 idadi imefikia 435

Kenya yarekodi visa 24 vya COVID-19 idadi imefikia 435

Tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha Korona siku hamsini na mbili zilizopita, Kenya leo imerekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi katika kipindi cha saa ishirini na nne pekee, ambayo ni ishirini na nne na kufikisha idadi ya walioambukizwa kuwa mia nne na thelathini na watano.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi, amesema miongoni mwa waliopimwa  Jijini Nairobi, kumi ni wa mtaa wa Eisleigh na saba wakiwa wa Kawangware. Aidha watano ni wa Mombasa huku wawili wakiwa wa eneo la Kuria Magharibi, hivyo kufanya kaunti ya Migori kuwa ya hivi punde zaidi kurekodi visa viwili vya kwanza vya maambukizi.

Mwangangi amesema watu wawili waliothibitishwa kuambukizwa korona, walirejea humu nchini kutoka Tanzania.

Hata hivyo, mtu mmoja amefariki dunia mjini Mombasa na kufikisha jumla ya walifariki kuwa ishirini na wawili. Kwa mujibu wa Mwangani, aliyefariki ni mwanamke wa umri wa miaka hamsini na mmoja na kwamba alikuwa na matatizo mengine ya kiafya.

Wakati uo huo, waliopona wamefikia mia moja hamsini na wawili baada ya wengine watano kupona na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Kwa sasa kuna jumla ya watu mia mbili kumi na wanne wanaoendelea kutibiwa Korona katika hospitali mbalimbali.

Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu katika Wizara ya Afya Daktari Patrick Amoth, amesema ni mmoja tu aliye kwenye hali mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Amoth amesema visa vya walioambukizwa nchini vitaongezeka hata zaidi ikizingatiwa kwamba serikali imeanza kuwapima watu kwa halaik, huku akionya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi hasa baada ya baadhi ya shughuli kuruhusiwa kurejelea.

Amoth amesema bado tiba kamili ya Korona haijapatikana licha ya baadhi dawa kama ile za kutibu Malaria na iliyotengenezwa kutibu Ebola ila haikuwahi kutumika kuidhinishwa katika majiribio hivyo kuwashauri Wakenya kuendelea kuwa waangalifu.