array(0) { } Radio Maisha | Watu 15 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona Kenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu 15 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona Kenya

Watu 15 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona Kenya

Watu kumi na watano wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini na kufikisha mia nne kumi na moja idadi jumla ya maambukizi nchini. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kumi na mmoja miongoni mwa kumi na watano hao ni wa Kaunti ya Mombasa, na wanne ni wa Kaunti ya Nairobi. Jumla ya watu elfu moja mia nne thelathini na nne wamepimwa  katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Wakati uo huo, watu sita zaidi wamethibitishwa kupona na kufikisha jumla ya waliopona kuwa mia moja hamsini.

Kwa mara ya kwanza watu wengi zaidi wamethibitishwa kufariki kutokana na korona ambao ni wanne hivyo kufikisha ishirini na mmoja jumla ya waliofariki dunia nchini.

Aidha imebainika kwamba miongoni mwa walioambukizwa wanawake wamekuwa wakipona haraka wakilinganishwa na wanaume, vile vile miongoni mwa waliofariki dunia wengi ni wanaume.

Waziri huyo amesema hatua ya serikali kuwaweka karantini kwa lazima watu waliorejea nchini kutoka mataifa ya nje mapema mwezi uliopita imesaidia pakubwa kudhibiti maambukizi zaidi. Amesema hali ingekuwa mbaya zaidi iwapo wangeruhusiwa kutangamana na jamii bila hali zao kufuatiliwa.

Kagwe amesema tayari serikali imeyatambua maeneo ambayo yameathirika zaidi akisema shughuli ya kuwatafuta watu waliotangamana na waathiriwa inaendelea. Kwa mfano amesema shughuli ya kuwapima watu kwa halaiki, mtaani kagwangware inaendelea mass testing ili kudhibiti hali.

Maeneo mengine ambayo yameathirika jijini Nairobi ni Kilimani, Kibra, Eastlegh na Pipeline.