array(0) { } Radio Maisha | Kagwe asisitiza hakuna fedha zilizoibwa huku Rais akisema ripoti itawekwa wazi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kagwe asisitiza hakuna fedha zilizoibwa huku Rais akisema ripoti itawekwa wazi

Kagwe asisitiza hakuna fedha zilizoibwa huku Rais akisema ripoti itawekwa wazi

Wizara ya afya imeendelea kujitetea dhidi ya matumizi mabaya ya shilingi bilioni 1.3 zilizotolewa na Benki ya Dunia kukabili janga la korona humu nchini

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesisitiza kwamba hakuna fedha zozote zilizotumiwa vibaya akitoa kuhakikisha kwamba fedha zote Wizara yake iliyotengewa zitatumika ifaavyo. Waziri Kagwe amesema ni rahisi kwa watu walio na nia mbaya na njama ya kuipata tope wizara yake kuitumia ripoti aliyowasilisha bungeni kudai kwamba kuna pesa ambazo zimeibwa.

Kagwe aidha ametetea matumizi ya shughuli nzima akisema yapo mahitaji mengi yanayostahili kushughulikiwa hivyo pesa nyingi zinaweza kutumika.

Awali Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa ripoti kuhusu matumizi ya fedha hizo itawekwa wazi kwa umma. Rais, amewashtumu wanaotumia janga la korona kuendeleza siasa duni, akisema wakati huu ni wa kuyaokoa maisha ya Wakenya. Akilihutubia taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Leba Dei amesisitiza  baada ya janga hili kukabiliwa ukaguzi utafanyika na ripoti itawekwa wazi kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Sehemu ya ripoti ilionesha kwamba shilingi milioni 42 zilitumika kukomboa ambulenzi kwa gharama ya shilingiu milioni 2.8 huku magari 30 pia yakitengewa shilingi milioni 14 kwa mafuta na ukarabati kwa gharama ya shilingi elfu 160 kwa mwezi ama shilingi elfu 40 kwa kwa wiki.

Katika bajeti hiyo pia shilingi milioni 10 zilitengewa chai japo ni shilingi milioni 4 tu zilizotumika kufikia sasa.