array(0) { } Radio Maisha | Babu awafunza watahiniwa wa KCSE Hisabati kupitia Facebook
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Babu awafunza watahiniwa wa KCSE Hisabati kupitia Facebook

Babu awafunza watahiniwa wa KCSE Hisabati kupitia Facebook

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino leo amewafunza watahiniwa wa Kidato cha Nnne KCSE somo na hisabati moja kwa moja kupitia mtandao wake wa Facebook

Babu ambaye amewashauri watahiniwa kufuatilia mafunzo hayo ili kuwasaidia katika mitihani yao inayotarajiwa baadaye mwaka huu.

Hatua ya Mbunge huyo inajiri wakati ambapo serikali imesema kwamba haina mpango wowote wa kuahirisha mitihani ya kitaifa na kwamba itaendela jinsi ilivyopangwa. Hapo jana Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa Nchini KICD ilisema mitihani ya mwaka huu itaangazia pahali ambapo wanafunzi wamefikia kuhusu masomo yao katika mtalaa.

Ni siku chache zilizopita Mbunge huyo aliibua mjadala mwingine katika mitandao ya kijamii wakati alipomwambia Waziri wa Elimu George Magoha akumpa karatasi za mitihani ya Kitaifa za mwaka huu ili athibitishe iwapo maswali yaliyomo ni kuhusu yale ambayo watahiniwa wamefunzwa mwaka huu.