×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rwanda yalegeza masharti ya kukabili Korona

Rwanda yalegeza masharti ya kukabili Korona

Serikali ya Rwanda imeondoa sitisho kamili la shughuli ambalo limekuwapo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Kufuatia kikao cha Baraza la Mawaziri nchini humo, kuanzia wiki ijayo, shughuli zote za binafsi na umma zitarejelewa japo kwa kuzingatia masharti ya kutokaribiana na kuvaa maski katika maeneo ya umma.

Hata hivyo mashirika ya binafasi na ya umma yametakiwa kuhakikishwa ni idadi ndogo tu ya watu wanaruhusiwa kuingia ofisni huku wengine wakifanyia kazi nyumbani.

Shughuli katika sekta ya ujenzi na utengenezaji bidhaa pia zitarejelewa. Mikahawa na hoteli itahudmu mchana tu huku masokoni wasimamizi wakitakiwa kuhakikisha kwamba ni asilimia 50 ya wauzaji wanaoruhusiwa kuendelea na biashara hiyo.

Uchukuzi wa umma na binafsi utarejelewa japo usafiri kati ya Mji Mkuu wa Kigali na mikoa mingine utasalia kusitishwa. Abiria katika magari ya uchukuzi wa umma pia watahitajika kuvaa maski na kuzingatia sharti la kutokaribiana.

Hata hivyo, licha ya hatua hizi shule zitasalia kufungwa hadi Septemba. Makanisa na maeneo ya ibada pia yatasalia kufungwa sawa na baa na biashara za mazoezi.

Pikipiki zitaendelea kubeba mizigo tu huku mikutano ya umma ikisalia kupigwa marufuku. Mipaka yote bado imefungwa isipokuwa kwa mizigo na Raia wa Rwanda wanaorejea nchini mwao na ambao watawekwa karantini ya lazima.

Ikumbukwe maambukizi nchini humo sasa ni 243. Hakuna aliyeaga dunia huku watu 104 wakipona.