array(0) { } Radio Maisha | Serikali kueleza matumizi ya shilingi bilioni moja kutoka benki ya dunia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali kueleza matumizi ya shilingi bilioni moja kutoka benki ya dunia

Serikali kueleza matumizi ya shilingi bilioni moja kutoka benki ya dunia

Serikali imeahidi kuwa itatoa ripoti kamili kuhusu matumizi ya shilingi bilioni moja ambazo ni ufadhili wa Benki ya Dunia katika kukabili maambukizi ya virusi vya korona.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Dakta Rashid Aman amesema maafisa wa uhasibu wanaendelea kulishughulikia suala hilo, na taarifa kamili itatolewa kesho.

Katika ripoti iliyowasilishwa na Wizara ya Afya kwa Kamati ya Bunge ya Afya, ilibainika kwamba shilingi milioni 42 zilitumika kukodi ambulenzi kwa gharama ya shilingi milioni 2.8 huku magari 30 pia yakitengewa shilingi milioni 14 kwa mafuta na ukarabati kwa gharama ya shilingi elfu 160 kwa mwezi ama shilingi elfu 40  kwa wiki.

Katika bajeti hiyo pia shilingi milioni 10 zilitengewa chai japo ni shilingi milioni 4 tu zilizotumika kufikia sasa. Shilingi milioni 70 ziliztumika kwa mawasiliano na nyingine shilingi milioni 11 kuwekaa mfumo wa kupokea simu bila malipo. Shilingi nyingine milioni 9 pia zilitumika kuchapisha fomu mbalimbali. Shilingi milioni 132 zilitengewa vifaa vya kujikinga, milioni 300 kwa mashine ya vipimo na nyingine milioni 196 kwa vifaa vya vipimo. Pia kuna mashine nyingine zilizotengewa shilingi milioni 98