array(0) { } Radio Maisha | Watu saba wafariki dunia kutokana na kipindupindu Marsabit
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu saba wafariki dunia kutokana na kipindupindu Marsabit

Watu saba wafariki dunia kutokana na kipindupindu Marsabit

Watu saba wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu katika Wadi ya Illeret Eneo Bunge la North Horr, kwenye Kaunti ya Marsabit.Mtoto mchanga ni miongoni mwa waliofariki dunia.

Watu wengine 137 waliokuwa wameathiriwa na kipindupindu wametibiwa na kuhuruhiswa kuondoka hospitalini.

Waziri wa Afya wa Kaunti hiyo Dakta Jama Wolde amesema miongoni mwa saba hao watano walifariki dunia wakiwa hospitalini huku wengine wakifariki dunia kwenye vijiji mbalimbali.

Wolde amesema waliofariki walikuwa na dalili za kipindupindu zikiwamo kuhara, kutapika na kupungukiwa na maji mwilini.
Inadaiwa kuwa mlipuko huo umetokea baada ya wakazi kutangamana na wakazi wa Bubua kutoka taifa la Ethiopita ambapo kuliripotiwa mlipuko huo wiki moja iliyopita.

Vituo viwili vya kushughulikia ugonjwa huo vimeanzishwa kwenye Wadi za Illeret na Teresagai kuwahudumia wakazi.

Wazira ya Afya humu nchini awali ilionya kwamba huenda Kaunti za Nairobi, Kajiado, Machakos, Garissa ,Narok, Nairobi na Kajiado zikakumbwa na mlipuko wa kipindupindu hasa wakati huu wa mvua kubwa.