array(0) { } Radio Maisha | Watu wanaokamatwa kwa kukiuka amri ya kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri wataachiliwa kwa dhama ya pesa taslim kabla ya kufikishwa mahakamani. Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakata Fred Mating'i amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila Mkenya anafuata maagizo yaliyotolewa na serikali katika kulikabili janga hili. Kauli ya yake inajiri huku watu kadhaa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu wanaokamatwa kwa kukiuka amri ya kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri wataachiliwa kwa dhama ya pesa taslim kabla ya kufikishwa mahakamani. Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakata Fred Mating'i amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila Mkenya anafuata maagizo yaliyotolewa na serikali katika kulikabili janga hili. Kauli ya yake inajiri huku watu kadhaa

Watu wanaokamatwa kwa kukiuka amri ya kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri wataachiliwa kwa dhama ya pesa taslim kabla ya kufikishwa mahakamani. Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakata Fred Mating'i amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila Mkenya anafuata maagizo yaliyotolewa na serikali katika kulikabili janga hili. Kauli ya yake inajiri huku watu kadhaa

Watu wanaokamatwa kwa kukiuka amri ya kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri wataachiliwa kwa dhama ya pesa taslim kabla ya kufikishwa mahakamani.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakata Fred Mating'i amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila Mkenya anafuata maagizo yaliyotolewa na serikali katika kulikabili janga hili.

Kauli ya yake inajiri huku watu kadhaa wakiwa tayari wamekamatwa na kuwekwa karantini kwa lazima hatua ambayo hata hivyo Gavana wa Isiolo Mohamed Kuti alisema huenda ikasababisha kuongezeka kwa visa vya maambukizi nchini. Aidha kumekuwapo na malalamishi kuhusu jinsi maafisa wa usalama wanavyowashughilikia wanaokiuka amri hiyo.

Ikumbukwe mahakama ilikataa kuizuia serikali kutekeleza amri hiyo baada ya ombi kuwasilishwa mahakamani.

Katika uamuzi huo, Jaji Weldon Korir badala yake alimtaka Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kuchapisha mwongozo kwenye magazeti rasmi la serikali kuhusu namna amri hiyo itakavyotekelezwa huku ikionya dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa utekelezaji wake.

Ombi hilo liliwasilishwa na Chama cha Wanasheria nchini LSK, kikisema amri hiyo inakiuka sheria.

Tayari Matiang'i ameagizwa na Seneti kufika mbele yake baada ya kukosa kufanya hivyo mara kadhaa kuieleza kuhusu mikakati ya usalama iliyowekwa katika kukabili korona.