array(0) { } Radio Maisha | Madereva wa migizo walalamikia msongamo Malaba
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Madereva wa migizo walalamikia msongamo Malaba

Madereva wa migizo walalamikia msongamo Malaba

Madereva wa magari ya mizigo ya masafa marefu wanaendelea kulalamikia kujikokota kwa mpango wa kuwapima ugonjwa wa Covid-19 kwa halaiki Mass Testing .

Licha ya serikali kusema kwamba madereva hao watanzaa kupimwa kwa misingi ya kuchangia kusambaa kwa virusi hivyo kwenye mataifa jirani hadi sasa shughuli hiyo haijaanza. Wakingumza na Radio Maisha, madereva hao wanaosafirisha bidhaa mbalimbali kwenye mataifa ya nje aidha wamelalamikia msongamano mkubwa wa magari kutoka mji wa Kanduyi hadi mpakani Malaba.

Madereva hao wamehusisha msongamano huo na uhaba wa wahudumu wa afya ambao wamewekwa mpakani Malaba kuwapima wanapoingia mpakani huku wakihofia maisha yao hasa nyakati za usiku.

Wametoa wito kwa Serikali ya Kenya na Uganda kuharikisha kuwapima na hata kushughulikia msongamano huo wakisema kwamba wamelazimika kusalia kwenye foleni licha ya kusafirisha gesi bidhaa ambayo haistahili kuwa kwenye foleni.

Msongamano huo umechangiwa na shughuli ya kuwapima  maradhi ya Covid-19 inayoondeshwa na Serikali ya Rais Yoweri Museveni huku wanaoingia Uganda wakiwa wale ambao wamepimwa na kuthibitisha hawajaambukizwa