×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Paka waambukizwa virusi vya korona - Marekani

Paka waambukizwa virusi vya korona - Marekani

Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Paka wawili nchini Marekani wamekuwa wanyama wa kwanza wa nyumbani kuambukizwa virusi vya korona. Paka hao wote wakiwa nchini New York walipimwa baada ya kuonesha dalili zinazofanana na za korona.

Paka alionesha dalili licha ya kuwa hakuna mtu yeyote katika nyumba anakoishi alikuwa ameambukizwa huku wa pili akipatikana na virusi katika boma ambapo mtu mmoja alikuwa ameambukizwa.

Hao si paka wa kwanza kuambukizwa korona, mapema mwezi jana wahudumu wa afya waligundua paka mmoja nchini Belgium aliyeambukizwa korona. Wahudumu hao walisema kwamba paka huyo aliambukizwa na mwenyewe aliyekuwa akiugua.

Nchini Uingereza wapenzi wa wanyama hao walionya kwani utafiti wa awali kutoka nchini uchina ulibainisha kwamba, paka ndio wanyama wanaoambukizwa virusi hivyo kutoka kwa binadamu kwa urahisi na wanaweza kuwaambukiza paka wenzao.

Paka hawa sasa wanaungana na wanyama wengine 8 wakiwamo simba na duma walioambukizwa.

Ikumbukwe nchini Kenya hakuna mnyama aliyeambukizwa japo Shirika la Uhifadhi Wanyama Pori tayari limeweka mikakati ya kuwalinda wanyama kufuatia uwezekano huo.