×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wabunge 17 miongoni mwa wanaugua Covid-19

Wabunge 17 miongoni mwa wanaugua Covid-19

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Taarifa ya Jumanne kwamba viongozi wa kisiasa 17 wakiwamo wabunge, maseneta na baadhi ya wafanyakazi wa bunge wanaugua maradhi ya Covid-19 yanaendelea kuibua hisia kinzani hususan kwenye mitandao ya kijamii.

Miongoni mwao ni wabunge waliopimwa wiki iliyopita na matokeo yao kutolewa Jumatatu wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea, maspika wa mabunge ya kitaifa na seneti walitakiwa kuahirisha mara moja vikao maalum vilivyokuwa vimeratibiwa kufanyika jana ili kuzuia maambukizi zaidi. Aidha, tumebaini kwamba zaidi ya wabunge 200 walijitolea kufanyiwa uchunguzi wa iwapo wanaugua virusi vya korona wakiwamo maspika Justin Muturi na Ken Lusaka.

Hata hivyo, Wizara ya Afya ambayo iliongoza shughuli hiyo, haijaweka wazi majina ya viongozi hao kwa mujibu wa takwa la sheria kuhusu kuwekwa wazi kwa hali ya afya ya mgonjwa.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kwamba kaunti za Kisii, Mandera, Kiambu na Machakos, ndizo za hivi punde zaidi kuathiriwa na maambukizi ya virusi hivyo huku watu kumi na wanne zaidi wakithibitishwa kuambukizwa vna kufikisha jumla ya visa mia moja sabini na viwili nchini.

Kupitia mtandao wa Twitter, chini ya alama ya reli #17Mps Wakenya wanatoa hisia kuhusu taarifa kuwa baadhi ya wabunge na maseneta wanaugua maradhi hayo hatari. Zaidi ya asilimia 99 waliochangia mjadala huo ambao unaongoza jukwaa masuala makuu nchini, wanaeleza jinsi korona imeleta usawa duniani...kwamba hakuna watakaosafirishwa katika mataifa yaliyopiga hatua katika masuala ya afya kama India na Uingereza. Sasa, wote wanaoambikizwa korona wanahaki hapa hapa, kutobiwa hapa hapa na kupona wakiwa hapa hapa.

 

Iwapo taarifa hizi ni za kweli, basi Wakenya wa kawaida kwa mara ya kwanza watatibiwa na waheshimiwa katika hospitali za humu nchini.

Aidha hapo ndipo viongozi hao watakapobaini hali halisi katika hospitali zetu...kwamba ni duni, kuna uchache wa vifaa na uchache wa wahudumu. Mwishowe, watabaini kwamba walifaa zamani zile kuboresha hali katika hospitali za humu chini badala ya kukimbia ughaibun kwenda kutibiwa.

Si kwamba tunawakeleji. Hapana. Tunasema tu kuwa ni wakati wa wao pia kujionea kazingira ambamo Wakenya wamekuwa wakitibiwa ili kujihukumu kwamba hawajawa wakifanya chochote kuboresha kupitia utungaji wa sheria.

Mwisho, kwa vile maspika wamekataa kuzungumzia suala hili, tunamwambia Waziri Kagwe aliyesema kuwa matangazo yote kuhusu korona yatolewe katika jukwaa moja la kitaifa ajitokeze wazi. Ajitokeze sawa na mataifa mengine mfano Uingireza ambayo imetoa tangazo kila saa kila dakika kuhusu hali ya Waziri Mkuu, Boris Johnson. Korona haijui kiongozi. Muhimu ni taarifa zote kuwekwa wazi.