array(0) { } Radio Maisha | KEMRI kurahisisha kupimwa kwa Covid-19
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

KEMRI kurahisisha kupimwa kwa Covid-19

KEMRI kurahisisha kupimwa kwa Covid-19

Na MIKE NYAGWOKA,

NAIROBI, KENYA, Taasisi ya Utafiti wa Matibabu, KEMRI inatarajiwa kurahisisha zaidi vipimo vya virusi vya korona na kuwawezesha wanaohofia kuugua kujipima wenyewe kufuatia mbinu mpya ya vipimo waliyobuni.

Taasisi hiyo imeanza kutengeneza vipimo vya haraka yaani rapid testing kit ambayo inafanana na mbinu inayotumika hivi sasa kupimwa uwapo wa virusi vya ukimwi au uja uzito ambapo sampuli inawekwa katika kifaa ambacho chini ya dakika chache kitaonesha iwapo mtu na virusi hivyo.  Prof Matilu ni mmoja wa watafiti.

Hata hivyo, kwasasa vipimo hivyo vitafanyika tu hospitalini ili kutimiza matakwa yote ya vipimo. Mbali na hayo mashine pia inayoweza kupima sampuli zaidi ya elfu 10 kwa siku inatarajiwa kuanza kutumika. Kwa sasa mashine zinazotumika zinqapima hadi sampului mia tatu kwa siku japo hivi punde zaidi, vituo zaidi vya kupima vimewekwa na kuongeza idadai hadi takriban mia 6 kwa siku.

Hatua hizi mbili zitaongeza idadi ya watu wanaopimwa kwa siku na vipimo vya halaiki yaani mass testing. Katika taarifa ya hivi punde zaidi ya Wizara ya Afya, takriban watu elfu 5 wamepimwa kufikia sasa.

Watu takriban 600 wamepimwa hivi punde zaidi huku watu 14 zaidi wakigunduliwa kuwa na virusi hivyo na kufikisha idadi ya walioambukizwa nchini kuwa watu 172.