array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya walioambukizwa korona nchini yafika 172

Idadi ya walioambukizwa korona nchini yafika 172

Idadi ya walioambukizwa korona nchini yafika 172

Watu kumi na wanne zaidi wameambukizwa virusi vya korona nchini. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kumi na wanne hao wanawajumuisha Wakenya kumi na wawili na raia wawili wa kigeni.

Akilihutubia taifa muda mchache uliopita, Kagwe amesema waathiriwa hao ni miongoni mwa watu mia sita tisini na sita waliopimwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

Watu wanne miongoni wa walioathibitishwa kuathirika leo hii walisafiri kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Muungano wa Milki za Kiarabu vilevile Marekani. Kwa jumla Kenya ina watu mia moja sabini na wawili walioambukizwa virusi vya korona kufikia sasa.

Wakati uo huo amethibitisha kupona kwa watu watatu waliokuwa wamewekwa karantini. Amesisitiza haja ya kila Mkenya kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali kulikabili janga la korona.

Waziri Kagwe amesisitiza agizo la Rais Uhuru Kenyatta la kuzuia usafiri wa kuingia na kutoka kwenye kaunti za Nairobi, Kilifi, Kwale na Mombasa  akisema hatua hiyo itasaidia pakubwa kudhibiti maambukizi sawa na ilivyofanyika katika mataifa mengine.