array(0) { } Radio Maisha | Gavana Mutua atishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia kwenye Kaunti ya Machakos

Gavana Mutua atishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia kwenye Kaunti ya Machakos

Gavana Mutua atishia kuweka marufuku ya kutoka na kuingia kwenye Kaunti ya Machakos

Gavana wa Machakos Dakta Alfred Mutua, amekuwa kiongozi wa hivi punde kuunga marufuku ya kutoka na kuingia kwenye  Kaunti za Nairobi, Kilifi, Mombasa na Kwale katika juhudi za kupambana na virusi vya korona.

Mutua amesema hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kukabili maambukizi ya korona.

Amesema Kaunti ya Machakos ikiwa miongoni mwa zile ambazo zitaathirika kutokana na marufuku hayo, amesema yu tayari kushiriana na serikali kufanikisha utekelezaji huo.

Mutua aidha,  amesema iwapo wakazi wa Machakos wataendelea kupuuza maagizo ya serikali ya kukabili korona , basi huenda pia yeye akaweka marufuku ya watu kuingia na kutoka, kwenye Kaunti ya Machakos.

Mutua ambaye ni Kinara wa Chama cha Maendeleo Chap Chap, aidha amewaonya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma na bodaboda dhidi ya kupuuza maagizo ya serikali ya kupunguza abiria kwa asilimia sitini kwamba watawajibishwa.