array(0) { } Radio Maisha | Kenya yaathirika zaidi na korona, Afrika Mashariki

Kenya yaathirika zaidi na korona, Afrika Mashariki

Kenya yaathirika zaidi na korona, Afrika Mashariki

Kenya bado inaendelea kuongoza Eneo la Afrika Mashariki kwa visa vingi vya maambukizi ya virusi vya korona vilevile visa vya vifo vinavyotokana na korona.

Takwimu za Wizara ya Afya nchini zinaonesha kuwa watu mia moja hamsini na wanane wameambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, baada ya visa vingine kumi na sita kuthibitishwa leo hii.

Rwanda ambayo ilichukua hatua za dharura mapema za kukabili korona kwa kufunga mipaka yake vilevile kusitisha safari za kimataifa za ndege, ndilo taifa la pili Afrika Mashari kwa idadi kubwa ya maambukizi ambayo sasa imefikia watu mia moja na wanne.

Nchini Uganda,  watu hamsini na wawili, wameambukizwa virusi hivyo huku kukiwa hakuna kisa chochote cha kifo ambacho kimeripotiwa.

Aidha taifa jirani la Tanzania,  limethibitisha visa vinne zaidi leo hii na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa  nchini humo kuwa ishirini na wanne.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,  Waziri wa Afya Ummi Mwalimu amewesema visa hivyo vinawahusisha watu wanaoishi jijini Dar es Salaam, Mwanza vilevile Zanzibar.

Wawili miongoni mwao ni mwanamume raia wa Tanzania wa Mwanza,  ambaye ni mfanyabiashara aliyeingia nchini humo kutoka Dubai.

Aidha mwathiriwa mwingine ni mwanamume mwenye umri wa miaka thelathini na mitano raia wa Tanzania, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika mataifa ya Bara Uropa, idadi ya walioambukizwa inaendelea kuongezeka. Nchini Uhispania, watu elfu mia moja thelathini na watano, na thelathini na wawili wameambukizwa virusi vya korona,  baada ya watu elfu tatu ,mia tatu themanini na sita kuthibitishwa leo hii. Aidha watu mia tano ishirini na wanane wameafariki dunia leo nchini humo.

Marekani, watu sabini na wanane zaidi wamefariki dunia katika muda wa saa kumi na tano zilizopita. Aidha watu elfu mia tatu thelathini na tisa,  mia moja thelathini na mmoja wameambukizwa virusi hivyo.

Kwa jumla, watu milioni moja, elfu mia mbili tisini na mbili, mia nne sabini na wawili  ambao wameambukizwa korona kote duniani, huku elfu mia mbili sabini na mbili, mia tano ishirini na tisa wakipona.