array(0) { } Radio Maisha | Wakenya 15 wakwama Qatar kwa kukosa usafiri

Wakenya 15 wakwama Qatar kwa kukosa usafiri

Wakenya 15 wakwama Qatar kwa kukosa usafiri

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Wakenya takriban 15 wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Hamad, Qatar baada ya kukosa ndege za kuwarejesha humu nchini. 

Hali hiyo imechangiwa na amri ya kutosalia nje iliyowekwa katika jiji kuu la Doha ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona. Baadhi ya Wakenya hao wamekwama katika uwanja huo kwa kipindi cha siku tatu sasa.

Ikumbukwe Kenya pia ilipiga marufuku safari zote za ndege za kimataifa ili kudhibiti hali ya maambukizi huku wote waliowasili nchini kabla ya marufuku hayo wakiwekwa karantini na serikali ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi endapo wameambukizwa.

Kufikia sasa, baadhi ya waliowekwa karantini ni miongoni mwa walioambukizwa.