×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika riadha Wilson Kipsang, akamatwa

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika riadha Wilson Kipsang, akamatwa

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Mwakilishi wa Wadi ya Kapchemutwa katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet Ambrose Kiplagat na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika riadha Wilson Kipsang, wamekesha korokoroni baada ya kukamatwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za kukiuka amri ya kutopatikana nje kati ya saa moja usiku na saa kumi na moja alfajiri.

Wawili hao pamoja na wengine zaidi ya kumi walikamatwa Alhamisi wakinywa pombe kwenye eneo moja la burudani mjini Iten mwendo wa saa mbili usiku.

Kabla ya kukamtwa kwao, kundi hilo lilizua vurugu likinga kukamatwa huku polisi wakilazimika kuwaita maafisa zaidi kuwasaidia kuwakabili.

Akithibitisha kisa hicho,  Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet John Mwinzi amesema kuwa walipokea ripoti kutoka kwa umma kuhusu washukiwa waliokuwa wamejifungia kwenye eneo moja la burudani.

Mwinzi hata hivyo,  amewaomba Wakenya kuendelea kufuata maagizo ya serikali ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.

Wote waliokamatwa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Iten wakitarajiwa kushtakiwa Ijumaa.