array(0) { } Radio Maisha | Familia moja katika Kaunti ya Mombasa yahitaji mchango wa kumzika jamaa yao aliyefariki kutokana na korona

Familia moja katika Kaunti ya Mombasa yahitaji mchango wa kumzika jamaa yao aliyefariki kutokana na korona

Familia moja katika Kaunti ya Mombasa yahitaji mchango wa kumzika jamaa yao aliyefariki kutokana na korona

Familia moja kwenye Kaunti ya Mombasa ambayo mwana wao alifariki dunia kutokana na virusi vya korona akiwa nchini Marekani, sasa imetoa wito kwa wahisani kuisaidia kuchangisha shilingi milioni 1.2 ili wamzike.

Askofu Elisha Juma na mkewe Mary Juma wa kanisa la Kenya Assemblies of God, eneo la Tudor wamesema kwamba wamepewa kipindi cha saa ishirini na nne kuuchukua mwili wa mwanao.

Marehemu alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita na alikuwa mhudumu wa afya katika hospitali ya St. Catherine of Siena jijini New York.

Ikumbukwe kuwa New York imetajwa kuwa miongoni mwa miji mikuu nchini Marekani ambako virusi hivyo vimeenea kwa kasi.