array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia virusi vya korona yafika zaidi ya elfu 47

Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia virusi vya korona yafika zaidi ya elfu 47

Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia virusi vya korona yafika zaidi ya elfu 47

Idadi ya watu waliofariki dunia kotokana na virusi vya korona imefikia watu 47,222 kufikia jana usiku, maambukizi yakiwa elfu 935,581 huku waliopona wakiwa watu elfu 194,260.

Taifa la Italy bado linaongoza na idadi kubwa zaidi ya watu waliofariki dunia, ambapo kufikia leo watu elfu 13,155 wamefariki dunia, ikifuatwa na Uhispania na 9,387, Marekani watu 5,109 na kisha Ufaranza  ambapo watu elfu nne na thelathini wamefariki dunia.

Hata hivyo, kwa kipindi cha saa ishirini na nne, Canada imerekodi idadi ya watu kumi na watano waliofariki dunia huku Marekani ikisema kuwa raia wake saba wamefariki dunia kutokana na korona huku bado ikiendelea kuongoza na idadi kubwa ya maambukizi.

Uchina chimbuko la virusi hivyo , ndilo taifa ambalo limetangaza idadi kubwa zaidi ya watu waliopona korona kufikia sasa, ambayo ni elfu 76, 238 huku watu elfu tatu , miatatu kumi na wawili wakiripotiwa kufariki dunia.

Barani Afrika, Aljeria bado inaongoza na vifo vya watu hamsini na wanane, ikifuatwa na Misri na hamsini na wawili, Morocco thelathini na tisa na kisha Burkina Faso ambapo watu kumi na sita wamefariki dunia.

Mataifa ya Senegal, Ghana, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi hivyo.

Haya yanajiri huku taasisi mbalimbali duniani ,  zikionya dhidi ya kuzuka kwa baa la njaa kutokana na maambukizi ya korona.