array(0) { } Radio Maisha | Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Raphael Mwana 'a Nzeki aaga dunia

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Raphael Mwana 'a Nzeki aaga dunia

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Raphael Mwana 'a Nzeki aaga dunia

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Raphael Ndingi Mwana 'a Nzeki amefariki dunia.

a'Nzeki ameaga dunia akiwa na umri wa miaka themanini na minane baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taarifa ya kifo chake imetangazwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki John Njue, ambaye amewashauri waumini na Wakenya kuiombea familia ya Ndingi kipindi hiki kigumu.

Kabla ya kifo chake, Ndingi alijihusishaa pakubwa na masuala ya uongozi wa taifa na hata wakati mmoja kuyaweka maisha yake hatarini, alipopinga unyanyasaji wa waathiriwa wa ghasia za kikabila katika eneo la Bonde la Ufa.

Aidha, aliyekuwa Katibu Msimamizi wakati wa uongozi wa a' Nzeki katika Kanisa la Holy Family Basilica kati ya mwaka 1998 hadi 2001, Lawrence Njoroge amesema, a' Nzeki alihakikisha Kanisa katoli linawekeza zaidi katika Sekta ya Elimu.

Lawrence ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Kasisi wa Kanisa Katoliki katika maeneo ya Machakos, Nakuru na Nairobi amesema, a' Nzeki alikuwa mpenda amani, umoja na utangamano. a' Nzeki alikuwa msomi wa masuala ya siasa na historia baada  ya kufuzu chuoni na shahada ya masuala ya siasa na historia.

Hii hapa sauti yake alipokuwa akifafanua mchango wa Kanisa Katoliki katika eneo la Isiolo.

Kanisa katolii hata hivyo, linatarajiwa kutoa ratiba kamili ya shughuli ya mazishi yake, ikizingatiwa maagizo ya serikali ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi,  wakati huu taifa linapokabili janga la korona.