array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya watu walioambukizwa visrusi vya korona nchini yafikia watu hamsini.

Idadi ya watu walioambukizwa visrusi vya korona nchini yafikia watu hamsini.

Idadi ya watu walioambukizwa visrusi vya korona nchini yafikia watu hamsini.

Idadi ya watu walioambukizwa visrusi vya korona nchini imeendelea kuongezeka na kufikia watu hamsini baada ya watu wanane zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo hatari vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Katika hotuba yake kwa taifa leo hii, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema shughuli ya kufuatilia hali ya afya ya watu elfu moja mia nne sabini na wanne inaendelea huku watu mia mbili thelathini na mmoja wakiruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kukamilisha muda wa siku kumi na nne wa karantini bila kuonesha dalili zozote za korona.

Amesema maafisa wa afya wanaendelea kuwafuatilia watu elfu moja mia mbili na kumi na mmoja wanaoaminika kutangamana na waathiriwa.

Kagwe amesema visa vya maambukizi vinawajumuishwa wakazi wa kaunti za Nairobi, Mombasa, na kaunti ya hivi punde kuwa na maambukizi hayo ikiwa ya Kitui. Amesema kaunti ya Nairobi sasa ina jumla ya visa thelathini na vinne, ikifuatwa na Kilifi kwa visa sita, Mombasa kwa visa vitatu, Kajiado na Kwale kisa kimoja kila kaunti vilevile Kitui.

Wakati uo huo Kagwe amesema ni wazi kwamba virusi hivyo vimeanza kusambaa miongoni mwa Wakenya. Amesema ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi, wahudumu wa bodaboda sasa ni sharti wabebe abiria mmoja pekee huku wakiwa wamevaa barakoa yaani Masks.

Kuhusu utekelezaji wa amri ya kutokuwa nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri, Kagwe amewashauri waajiri kuwaachilia wafanyakazi wao kufikia saa kumi jioni ili kufanikisha mpango huo.

Taarifa ya Kagwe inajiri saa chache tu baada ya Tanzania kuthibitisha visa vitano zaidi na kufikisha jumla ya visa kumi na tisa nchini humo.