array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Nyali apendekeza kikao cha dharura bungeni

Mbunge wa Nyali apendekeza kikao cha dharura bungeni

Mbunge wa Nyali apendekeza kikao cha dharura bungeni

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Ikiwa njia mojawapo ya kuhakikisha wananchi walala hoi hawaathiriki zaidi na kuzorota kwa uchumi kutokana na maambukizi ya virusi vya korona, Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amemwandikia Kiongozi wa Wengi Bungeni Aden Duale akimtaka kuitisha kikao cha dharura cha wabunge.

Katika barua iliyowasilishwa bungeni mapema leo, Mbunge huyo amemtaka Duale kuitisha kika maalum kujadili mbinu zinazoweza kutumiwa kuwakinga wananchi dhidi ya athari za virusi hivyo hatari.

Aidha, kupitia barua hiyo, Ali ambaye maarufu Jicho Pevu amelikumbusha bunge kwamba lina jukumu la kuwatetea na kuwalinda wananchi ambao ni wapigakura dhidi ya mfumuko wa bei ya bidhaa za msingi pamoja kupitisha bajeti maalum itakayowafaa wananchi kwa kipindi hiki.