array(0) { } Radio Maisha | Marekani yaongoza kwa maambukizi ya virusi vya korona

Marekani yaongoza kwa maambukizi ya virusi vya korona

Marekani yaongoza kwa maambukizi ya virusi vya korona

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Taifa la Marekani, ndilo sasa linaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ya korona kote duniani.

Kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Hopkins, Marekani ina jumla ya watu elfu themanini na mbili mia nne walioambukizwa Korona, ikilinganishwa na elfu themanini na moja mia saba wa uchina na elfu thelamini mia tano wa Italia.

Hata hivyo, Italia inaendelea kuongozwa kwa idadi ya vifo, ambavyo sasa vimefikia elfu nane mia mbili, huku idadi ya waliofariki dunia Marekani ikiwa zaidi ya elfu moja.

Nchini Uchina,  jumla ya watu elfu tatu mia mbili tisini na wawili wamefariki dunia tangu virusi hivyo kuripotiwa mwaka jana. Aidha Uchina imerekodi visa vingine hamsini na vitano vya maambukizi ya Korona, hamsini na vinne vikiwahusisha watu wanaoingia  nchini humo kutoka mataifa ya kigeni huku mmoja akiambukizwa nchini humo. Jiji la Hubei ndilo limeathirika zaidi.

Barani Afrika;  Afrika Kusini ndiyo inayoongoza kwa visa vya korona ambavyo sasa vimefikia, mia tisa ishirini na saba.

Duniani kote idadi ya walioambukizwa imefikia elfu mia tano thelathini na moja mia nane sitini na nne huku watu elfu ishirini na nne na sabini na tatu wakifariki dunia.