array(0) { } Radio Maisha | Bunge la Seneti kufanya kikao cha dharura Jumanne kujadili suala la korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Bunge la Seneti kufanya kikao cha dharura Jumanne kujadili suala la korona

Bunge la Seneti kufanya kikao cha dharura Jumanne kujadili suala la korona

Bunge la Seneti linatarajiwa kufanya kikao cha dharura Jumanne wiki ijayo ili kuidhinisha mikakati iliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta jana alipohutubia taifa kuhusu janga la virusi vya korona nchini.

Haya yanajiri huku maspika Ken Lusaka wa Seneti na Justin Muturi wa Bunge la Kitaifa wakifanya mkutano leo hii ambapo wamekubaliana kukatwa asilimia thelathini ya mishahara yao kuwekwa katika hazina ya kukabili maambukizi ya korona.

Kwa mujibu wa Spika Lusaka, pesa hizo zitakatwa kwa muda wa miezi mitatu ijayo au hata zaidi kutegemea na jinsi serikali itakavyojikakamua kukabili virusi hivyo.

Hata hivyo, Lusaka amesema hakuna mbunge au seneta atakayelazimishwa kufanya hivyo, kwani watakaokubali kukatwa mishahara yao watafanya hivyo kwa hiari.

Kwa upande wake Spika Muturi, ameiomba Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika katika kukabili virusi hivyo.

Tayari Rais Kenyatta, Naibu wake William Ruto, mawaziri na makatibu wamekubali kukatwa mishahara yao. Iwapo agizo hilo litatekelezwa, Rais ambaye hupokea shilingi milioni 1.44 kila mwezi atapokea shilingi elfu 288, 000 huku naibu wake ambaye hulipwa shilingi milioni 1.22 akipokea shilingi elfu 245,000.

Mawaziri ambao kwasasa hupokea mshahara wa shilingi  elfu 924,000 kila mwezi, watapokea shilingi elfu 646,000 ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya rais na naibu wake.

Wakati uo huo, baadhi ya wabunge akiwamo Babu Owino wa Embakasi Mashariki na Seneta Maalumu Millicent Omanga wamekubali kukatwa mishahara yao. Babu katika mtandao wake wa Facebook, ametangaza kwamba amekubali asilimia hamsini ya mshahara wake kugharimia matibabu ya wagonjwa wa korona. Aidha, Omanga alichapisha kwamba asilimia sitini ya mshahara wake utumike vivyo hivyo.