array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi wa miaka 19 athibitishwa kuugua korona Kakamega

Mwanafunzi wa miaka 19 athibitishwa kuugua korona Kakamega

Mwanafunzi wa miaka 19 athibitishwa kuugua korona Kakamega

Mwanafunzi mwenye umri miaka kumi na tisa aliyerejea nchini kutoka Uswizi amethibitishwa kuwa na korona. Kisa hiki kinafikisha idadi ya walioambukizwa nchini ishirini na tisa.

Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya  amesema mwanafunzi huyo pamoja na mhudumu wa bodaboda aliyembeba wamewekwa karantini.

Aidha jamaa wa mwanafunzi huyo wanafanyiwa ukaguzi ili kubaini iwapo wameambukizwa. Gavana Oparanya vile vile amesema mwakilishi mmoja wa wadi ni miongoni mwa watu wanne ambao wameshauriwa kujiweka karantini kwa kutangamana na mwathiriwa huyo.

Kando la suala la waathiriwa hao, Oparanya amewaagiza wafanyakazi wa serikali ya kaunti kusalia nyumbani kwa siku kumi na tano ili kudhibiti maambukizi.

Wakati uo huo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe anatarajiwa kuwahutubia wanahabari wakati wowote kuanzia sasa kuhusu suala lilo hilo la korona.