array(0) { } Radio Maisha | Joho amesema wasiojiweza katika kaunti ya Mombasa watakabidhiwafedha za kujikidhi

Joho amesema wasiojiweza katika kaunti ya Mombasa watakabidhiwafedha za kujikidhi

Joho amesema wasiojiweza katika kaunti ya Mombasa watakabidhiwafedha za kujikidhi

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amesema kwamba serikali yake imetenga kima cha shilingi milioni mia mbili za kuyakidhi mahitaji ya familia zisizojiweza endapo marufuku ya kutotoka nje yatatekelezwa kikamilifu.

Akizungumza muda mfupi uliopita Joho amesema kwamba kila mkazi wa kaunti hiyo atasambaziwa kiwago fulani cha fedha za kukidhi mahitaji yake.

Amesema kwamba kamati maalum inayojumuisha sekta binafsi itakayoongozwa na Abdhul Sanji imebuniwa ili kuhakikisha lengo hilo linaafikiwa.

Amewahimiza wahisani kujitokeza na kutoa msaada wa vyakula katika Shule ya Msingi ya Tom Mboya ambayo imetengwa katika ukusanyaji wa msaada huo.

Vilevile amewaonya wafanyabiashara wa vyakula dhidi ya kuongeza bei kwani watakabiliwa kisheria.


Ameliagiza bunge la kaunti hiyo kufanya kikao cha dharura kujadili jinsi ambavyo litashirikana na serikali hiyo kufanikisha lengo hilo.

Kwa upande wake Kamishna wa Kaunti hiyo Gilbert Kitio amesisitiza wakazi wa Mombasa kusalia majumbani ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya korona.