array(0) { } Radio Maisha | Mhubiri mmoja katika Kaunti ya Kitui atakiwa kuzingatia masharti ya kujiweka karantini

Mhubiri mmoja katika Kaunti ya Kitui atakiwa kuzingatia masharti ya kujiweka karantini

Mhubiri mmoja katika Kaunti ya Kitui atakiwa kuzingatia masharti ya kujiweka karantini

Mhubiri mmoja wa Kanisa Katoliki kwenye Kaunti ya Kitui ameagizwa kuzingatia masharti ya kujiweka karantini baada ya kuonekana mitaani licha ya kurejea nchini tarehe 23 kutoka Italia. Inaarifiwa kwamba mhubiri huyo kwa jina Nicholas Maanzo alirejea nchini siku ya Jumatatu wiki hii huku akionekana katika duka moja kuu siku ya Jumanne mjini Kitui na baadaye kuelekea katika mashine ya ATM.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Upelelezi, DCI katika eneo la Kitui ya Kati, Nzioka Singi, hapo jana aliandamana na maafisa wa afya hadi nyumbani kwa mhubiri huyo katika eneo la Kihara ambapo alipimwa na kubainika hakuwa na dalili zozote za virusi vya korona japo ameagizwa kuendelea kujiweka karantini hadi atakapokamilisha muda wa siku 14.

Mhubiri huyo anadai sababu zilizomfanya kuondoka nyumbani ni kwa kuwa hakuwa na chakula japo ameahidi kuzingatia masharti. Ikumbukwe askofu mmoja wa Kanisa Katoliki ni miongoni mwa watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona huku watu waliotangamana naye wakihitajika kufanyiwa uchunguzi. Tayari baadhi wamepimwa na wanasubiri matokeo.