array(0) { } Radio Maisha | Wetangula aitaka serikali kuisaidia sekta ya juakali wakati huu wa janga la korona

Wetangula aitaka serikali kuisaidia sekta ya juakali wakati huu wa janga la korona

Wetangula aitaka serikali kuisaidia sekta ya juakali wakati huu wa janga la korona

Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula  ameitaka serikali kuweka mikakati maalum ya kusaidia uchumi wa sekta ya juakali na kilimo msimu huu wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.

Wetangula amesema ipo  haja ya serikali kuwapa wakulima pembejeo na usaidizi zaidi ili kuwezesha taifa kujitegemea kilimo ikizingatiwa mataifa mengi yanayotegemewa kuzalisha vyakula yameadhirika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, seneta huyo wa Bungoma licha ya kusifia uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta hapo jana , ametoa changamoto kwa serikali kupiga jeki sekta ya juakali inayotoa ajira kwa idadi kubwa kwa wakenya mbali na kuitaka serikali  kuwapa wakenya vyakula iwapo taifa litasitisha shughuli zote za lockdown

Vile vile amelitaka Bunge lirejelee vikao ili kuangazia maswala muhimu kuhusu  janga la korona.