array(0) { } Radio Maisha | erikali ya Kaunti ya Kilifi imetangaza marufuku ya magari yote ya usafiri wa umma

erikali ya Kaunti ya Kilifi imetangaza marufuku ya magari yote ya usafiri wa umma

erikali ya Kaunti ya Kilifi imetangaza marufuku ya magari yote ya usafiri wa umma

Serikali ya Kaunti ya Kilifi imetangaza marufuku ya magari yote ya usafiri wa umma kuingia na kutoka katika kaunti hiyo kuanzia kesho Ijumaa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari gavana wa Kaunti hiyo Amason Jefwa Kingi amesema kwamba agizo hilo litaanza kutekelezwa saa kumi na moja asubuhi.

Amesema kwamba agizo hilo litaendelea hadi wakati ambapo tangazo la kusitishwa kwake litakapotolewa. Kwa wamiliki wa magari ya binafsi, Kingi amewagiza kuhakikisha watu wanaoabiri magari hayo wanaketi bila kukaribiana.

Agizo lingine ambalo Kingi ametangaza ni marufuku kwa vituo vya kuchinjia nyama vilevile maeneo ya kuuza nyama. Shughuli za uchuuzi pia zimepigwa marufuku. Serikali hiyo vilevile imeagiza kufungwa mara moja kwa chimbo zote zilizo katika kaunti hiyo.

Kingi amesema kwamba magizo haya ni ya kuwaepusha wakazi wa kaunti hiyo ambayo ni miongoni mwa zilizotangazwa kuathiriwa na virusi vya korona kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa.