array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta apongezwa kwa mikakati aliyoweka kuzuia korona

Rais Kenyatta apongezwa kwa mikakati aliyoweka kuzuia korona

Rais Kenyatta apongezwa kwa mikakati aliyoweka kuzuia korona

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa hatua alizotangaza jana za kuwasaidia Wakenya wakati huu wa ugumu wa uchumi kufuatia marufuku ambayo yamewekwa kwa lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya Korona.

Mutua amempongeza kwa kupunguza kodi  inayotozwa Wakenya akisema hilo litasaidia watu wenye mapato ya chini huku akiwashauri kuzingatia maagizo yaliyotolewa na Wizara ya Afya kujikinga dhidi ya maambukizi.

Mutua aidha ameeleza kuwa magavana wengine wa humu nchini watafanya mkutano kukubaliana jinsi ya kupunguza mishahara yao jinsi Rais Kenyatta alivyotangaza kukatwa kwa asilimia 80 ya mshahara wake.