array(0) { } Radio Maisha | Waziri Macharia awapiga marufuku watu wanaotembea kwa miguu kutumia kivuko cha Likoni

Waziri Macharia awapiga marufuku watu wanaotembea kwa miguu kutumia kivuko cha Likoni

Waziri Macharia awapiga marufuku watu wanaotembea kwa miguu kutumia kivuko cha Likoni

Waziri wa Uchukuzi, James Macharia amewapiga marufuku watu wanaotembea kwa miguu dhidi ya kutumia Kivuko cha Likoni katika kipindi cha siku telathini zijazo. Waziri huyo amesema watakaotaka kuvuka kutumia kivuko hicho basi watahitajika kupanda kgari, akisema hatua hiyo itazuia msongamano wa watu.

Ikumbukwe mapema leo watu wenye dalili za homa walizuiwa kuabiri feri kwenye kivuko cha Likoni Kaunti ya Mombasa.

Kwa mujibu wa Kamati ya Kushughulikia Majanga kwenye Serikali ya Kaunti hiyo, hatua hiyo itachangia pakubwa kupunguzwa kwa visa vya kuambukizwa kwa virusi vya korona miongoni mwa wanaotumia vyombo hivyo vya usafiri.

Waliokuwa na dalili za homa walishauriwa, kutafuta huduma katika hospitali zilizokuwa karibu.

Tukiachana na ya humu nchini ni kwamba China imetangaa kurejelea safari za ndege kutoka na kuelekea jijini Wuhan lililoathirika zaidi ya virusi vya korona. Safari hizo ambazo zitakuwa za nchini humo pekee zitarejelewa kuanzia Aprili tarehe 8.