array(0) { } Radio Maisha | Raia wa Marekani wapewa nafasi ya kuondoka humu nchini

Raia wa Marekani wapewa nafasi ya kuondoka humu nchini

Raia wa Marekani wapewa nafasi ya kuondoka humu nchini

Ubalozi wa Marekani humu nchini umewapa raia wake wanaoishi Kenya nafasi ya mwisho kuondoka mara moja wakati ambapo visa vya maambukizi ya virusi vya korona vimeongezeka na kufikia 25.

Shirika la Ndege la Kenya Airways, limesema kwamba litawasafirisha raia wa Marekani leo Jumatano ambayo ni siku ya mwisho kwa safari zake za kimataifa katika harakati za kuzuia maambukizi ya korona.

Ubalozi  huo ,umewataka raia wake kutumia fursa hiyo kabla ya usiku wa manane kurejea Marekani. Raia hao wametakiwa kuwasiliana na uongozi wa KQ kabla ya saa tisa alasiri.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya Shirika la Ndege la Uingereza kuanzisha safari za ndege hadi London kuwasafirisha raia wake walioko nchini.

Balozi wa Uingereza nchini, Jane Mariott amewataka raia wa taifa hilo kutembelea ubalozi huo ili kukata tiketi.