array(0) { } Radio Maisha | Wanaotumia kivuko cha Likoni wakosa kutumia barakoa

Wanaotumia kivuko cha Likoni wakosa kutumia barakoa

Wanaotumia kivuko cha Likoni wakosa kutumia barakoa

Asilimia kubwa ya watu wanaotumia Kivuko cha Likoni kwenye Kaunti ya Mombasa wamekosa kufuata agizo lililotolewa jana na Mshiriki wa Utawala eneo la Pwani John Elungata la kila anayetumia feri kuvalia barakoa ya kufunika uso na mdomo.

Wakizungumza na kituo hiki wamesema kwamba wengi wao wanategemea kazi za jua kali  kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo itakuwa vigumu kwao kununua barakoa ama vitambaa vya mkono jinsi ilivyoagizwa.

Wameishinikiza serikali kusambaza vifaa hivyo katika Kivuko hicho ili kuhakikisha kila anayevuka anapewa hivyo kuzuia kusambaa zaidi kwa Ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yanajiri huku biashara ya uuzaji wa barakoa na vitamba vya mkono ikiendelea kunoga kwenye ng’ambo zote mbili za kivuko hicho.