array(0) { } Radio Maisha | Italia yatishia kuwafunga jela wanaokosa kujiweka karantini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Italia yatishia kuwafunga jela wanaokosa kujiweka karantini

Italia yatishia kuwafunga jela wanaokosa kujiweka karantini

Taifa la Italia limetishia kuwafunga jela waathiriwa wa virusi vya korona watakaokiuka agizo la kujiweka karantini ili kuthibiti maambikizi zaidi.

- Waathiriwa ambao hatatajiweka karantini kwa muda wa siku kumi na nne inavyostahili watafungwa jela kwa miaka mitano.

- Wanaokiuka agizo la kukaa nyumbani baada ya shughuli zote kusitishwa watatozwa faini ya uro elfu tatu au dola elfu tatu mia mbili arubaini na tano ambazo ni zaidi ya shilingi laki tatu zakenya.

- Biashara zitakazokiuka maagizo hayo zitakuwa kwa kati ya siku tano na thelathini.

- Maagizo hayo yatafanyiwa marekebisho kila mwezi hadi Julai tarehe 31.


Itali ambalo ni taifa linaloendelea kuathirika zaidi na maambukizi ya Korona limerekodi zaidi ya vifo va watu elfu saba na wengine zaidio ya elfu sabini wakiambukizwa.

Wakati uo huo, Waziri Mkuu wa Uchina Li Keqiang amewaonya maafisa nchini humu dhidi ya kuficha takwimu za mamabukizi mapya baada a taifa hilo kutorekodi mamabukizo yoyote kwa siku kadhaa. Kequiang amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanakuwa na imani na serikali katika kukabili maambukizi zaidi.

Nchini India madaktari wamefurushwa kutoka makazi yao huku wananchi wkaihofia kwamba watawaambukiza virusi hivyo. Inadaiwa madaktari wanaoishi kwenye mitaa miongoni mwa wananchi wamekuwa wakibaguliwa na kunyanyaswa ikidaiwa kwamba wanaweza kuwaambukiza korona kwani wanawashughulikia wagonjwa hospitalini. India ambayo imerejkkodi visa mia tano hamsini na viwili ilisitisha shughuli zote kuanzia usiku wa manane leo