array(0) { } Radio Maisha | Maambukizi ya Korona yafika zaidi ya mia saba nchini Afrika Kusini

Maambukizi ya Korona yafika zaidi ya mia saba nchini Afrika Kusini

Maambukizi ya Korona yafika zaidi ya mia saba nchini Afrika Kusini

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona nchini Afrika Kusini imefikia mia saba na tisa kutoka mia tano hamsini na nne hapo jana. 

 Waziri wa Afya Zweli Mukhinze amesema  visa vingine mia moja hamsini na vitano vimethibitishwa kufikia leo hii.

Mukhinze amesema huenda idadi ya maambukizi ikazidi licha ya kusitisha shughuli zote.

Kwingineko taifa la Newzealand limetangaa hali ya hatari huku likiana mpango wa kusitisha shughuli zote. waziri Mkuu Jacinta Ardern amesema hakuna atakayeruhusiwa kutoka nje kuanzia usiku wa manene leo hii, ili kuzuia maambukizi ziadi.

Baani Afrika Mataifa ambayo yametangaza hali ya hatari ni Jmauhuru ya Kidemokrasi ya Congo, Sierra Leon na Ivory Coast. Aidha jumla ya watu sitini na wawili barani Afrika wamefariki dunia na wengine elfu mbili mi moja thelathini na saba wakiambukizwa.

Duniani idadi ya waliofariki imefikia zaidi ya elfu kumi na nane huku wengine elfu mia nne na nne wakiambukizwa.