array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya maambukizi ya Virusi vya Korona nchini yafika 25

Idadi ya maambukizi ya Virusi vya Korona nchini yafika 25

Idadi ya maambukizi ya Virusi vya Korona nchini yafika 25

Watu wengine tisa wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini na kufikisha 25 idadi ya maambukizi nchini. Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe, miongoni mwa tisa hao, saba ni Wakenya huku wawili wakiwa raia wa kigeni. Aidha, watatu miongoni mwa Wakenya walioambukizwa ni wale waliotangamana na watu walioambukizwa awali. Walioathiriwa aidha ni watu wa kaunti nne ambazo ni Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale. Amezitaja kaunti hizi nne kuwa zenye hatari ya kukumbwa na maambukizi zaidi.

Waziri Kagwe aidha amesema watu 745 wanaendelea kufuatiliwa kwa kutangana na walioathirika huku waliotangamana na walioambukizwa wanaendelea kutafutwa. Kutokana na ongezeko la maambukizi, Waziri Kagwe amesema hapo kesho serikali itatangaza mikakati zaidi ambayo itawekwa ili kukabili hali.

Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa hoteli ambako watu wanaorejea nchini wanawekwa karantini, kutowatoza ada za juu kipindi hiki. Ametoa hakikisho kwamba utaratibu wa kuwaweka karantini wanaoingia nchini umeboreshwa baada ya changamoto kushuhudiwa awali. Wakati uo huo, Waziri amesema ni habari njema kwamba hali za watu ambao waliambukizwa awali na ambao amesema hali yao inaendelea kuimarika.