array(0) { } Radio Maisha | Serikali yatenga maeneo 57 ya kujiweka karantini

Serikali yatenga maeneo 57 ya kujiweka karantini

Serikali yatenga maeneo 57 ya kujiweka karantini

Serikali imeyaorodhesha maeneo 57 ambayo wananchi hasa wanaoingia kutoka mataifa ya nje wanaweza kuyatumia kujiweka karantini wakati huu ambapo janga la virusi vya korona linaendelea kushuhudiwa.

Miongoni mwa maeneo hayo ni  Hoteli ya Hill Park iliyo katika Mtaa wa Upperhill, Hilton Garden Inn iliyoko katika Uwanja wa Ndege wa JKIA,  Safari Park, Pride Inn Hotels, Jacaranda Hotel, Trademark Hotel, Four points Sheraton na Boma Hotel. Maeneo mengine yapo katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya School of Government, Crown Plaza airport, Mombasa beach hotel na Lamada hotel.

Ikumbukwe baadhi ya watu walioingia nchini jana walilalamikia kutopewa taarifa za kina na serikali kuhusu maeneo ya kujiweka karantini huku wakidai baadhi ya hoteli walizoagizwa kutatufa hifadhi zilikuwa zikiitisha kiasi kikubwa cha fedha. Hata hivyo Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe alizitaka hoteli hizo kujali maslahi ya wanaotafuta huduma huko na kutowalipisha kiasi kikubwa cha fedha wakati huu mgumu.

Serikali iliagiza kwamba wote wanaorejea nchini watatengwa katika maeneo maalum kwa kipindi cha siku 14 ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kubainika kwamba watu kadhaa wamekuwa wakikiuka maagizo ya kujitenga.