array(0) { } Radio Maisha | Barakoa za Jeshi la Ujerumani zaripotiwa kutoweka katika Uwanja wa JKIA

Barakoa za Jeshi la Ujerumani zaripotiwa kutoweka katika Uwanja wa JKIA

Barakoa za Jeshi la Ujerumani zaripotiwa kutoweka katika Uwanja wa JKIA

Barakoa, facemasks takriban milioni sita za Jeshi la Ujerumani zimeripotiwa kutoweka katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA. Barakoa hizo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea Ujerumani.

Wizara ya Ulinzi ya Jiji la Berlin, Ujerumani imesema inajaribu kutegua kitendawili kuhusu namba barakoa hizo zilivyotoweka. Bidhaa hizo zilistahili kuwasili barani Uropa Machi 20 ili kutumiwa kuwakinga watu dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Korona.

Kufikia sasa taifa la Ujerumani lina visa e;fu thelathini, mia moja hamsini vya maambukizi ambapo miongoni mwa visa hivyo, elfu moja tisini na vinne ni vipya. Aidha watu 130 wamefariki dunia nchini humo, visa saba vikiwa vya hivi punde.