array(0) { } Radio Maisha | Kaunti ya Nairobi yaondoa ada za kuhjifadhi mili

Kaunti ya Nairobi yaondoa ada za kuhjifadhi mili

Kaunti ya Nairobi yaondoa ada za kuhjifadhi mili

Serikali ya Kaunti ya Nairobi imeondoa ada zote za kuhifadhi mili katika vyumba vyote vya wafu, amesema Waziri wa Afya Hitan Majivdia kwenye kaunti hii.

Ameongezea kwamba agizo hilo litadumu kwa kipindi cha siku saba japo mili ambayo inaendelea kuhifadhiwa kufuatia kesi mahakamani itasalia.

Majivdia aidha amesema tayari mikahawa mbalimbali jijini Nairobi imeanza kuzingatia agizo la kuwauzia wateja vyakula kisha kuondoka yaani takeaway services ili kuzuia maambukizi.

Wakati uo huo, wahisani wameombwa kuchangia juhudi za ununuzi wa vifaa vya kuosha mikono na kuvisambaza katika maeneo mbalimbali huku kukiwa na wale ambao tayari wamesambaza vifaa hivyo maeneo ya jiji la Nairobi na katika reli ya kisasa, SGR.