array(0) { } Radio Maisha | Mtawa wa Kanisa Katoliki, Makueni awekwa karanti kwa lazima

Mtawa wa Kanisa Katoliki, Makueni awekwa karanti kwa lazima

Mtawa wa Kanisa Katoliki, Makueni awekwa karanti kwa lazima

Mtawa wa Kanisa Katoliki wa Makueni ambaye ameingia nchini hivi maajuzi kutoka Uhispania amewekwa karantini kwa lazima kwa kipindi cha majuma mawili kwa mujibu wa agizo la Wizara ya Afya, baada ya kupuuza kufanya hivyo. Mtawa huyo aliingia nchini Machi 18.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameagiza kwamba kila anayewasili nchini ajiweka karantini kwa gharama yake mwenyewe, ili kuzuia maambukizi ya korona. Atakayekiuka sharti hilo atazuiwa kwa siku 14 kwa lazima kisha kushtakiwa.

Mtawa huyo ambaye pia ni muuguzi anasemekana kupokelewa na wazazi wake, ndugu zake wawili na muuguzi mwenzake wa Machakos. Amewekwa karantini baada ya wakazi kuwasilisha malalamishi kwa maafisa wa polisi kumhusu.

Kenya imeimarisha mikakati ya kukabili virusi vya korona huku jumla ya walioambukizwa wakiwa 16.