array(0) { } Radio Maisha | Msaada wa Jack Ma wa vifaa vya kukabili Virusi vya Korona wawasili

Msaada wa Jack Ma wa vifaa vya kukabili Virusi vya Korona wawasili

Msaada wa Jack Ma wa vifaa vya kukabili Virusi vya Korona wawasili

Msaada wa vifaa vya kupimia virusi vya korona, vilevile vya kujikinga wakati wa kuwashughulikia wagonjwa wanapokuwa karantini uliotolewa na Wakfu wa Jack Ma umewasili dakika chache zilizopita katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JKIA.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Afya Daktari Patrick Amoth amesema vifaa hivyo ni zaidi ya elfu ishirini.

Amoth amesema vifaa hivyo vitasambazwa katika vituo vya kuwahudumia waathiriwa wa virusi vya korona vilevile kwenye kaunti mbalimbali ili kufanikisha juhudi za kukabili virusi hivyo hatari.

Kenya sasa inakuwa nchi ya tano kupokea vifaa hivyo tangu vilipowasilishwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mataifa mengine yaliyopokea vifaa hivyo ni, Misri, Djibout , Eritrea, na Sudan.

Msaada huu unajiri baada ya wakfu huo kuisadia Marekani na vifaa elfu mia tano vya kupimia korona lengo likiwa kukabili virusi hivyo duniani.