array(0) { } Radio Maisha | Kenya kutumia dola bilioni nane kukabili maambukizi ya virusi vya korona

Kenya kutumia dola bilioni nane kukabili maambukizi ya virusi vya korona

Kenya kutumia dola bilioni nane kukabili maambukizi ya virusi vya korona

Kenya ina hifadhi ya kima cha bilioni nane, dollar za Marekani ambazo zitatumika kulisaidia taifa hili wakati huu ambapo linakabiliwa na maambukizi ya virusi vya korona.

Akiwahutubia wanahabari kupitia mtandao wa Youtube, Gavana wa Benki Kuu Patrick Njoroge amesema kwamba miongoni mwa mikakati ambayo wameweka ni kutuma ombi la msaada kwa Benki ya Dunia kutoa ufadhili wa kuisaidia Wizara ya fedha kutimiza malengo yake katika kuvikabili virusi hivyo.

Aidha, Njoroge amesema kwamba huenda uchumi wa Kenya ukakua kwa asilimia ndogo ya 3.4 mwaka huu kinyume na asilimia 6.2 ilivyokusudiwa mwaka huu kufuatia athari ya virusi vya korona ambavyo vimeathiri sekta ya uchumi pakubwa.

Njoroge aidha amekiri kuendelea kuathirika kwa biashara ya usafirishaji wa bidhaa hadi mataifa mengine hasa maua akisema marufuku ya safari za ndege hadi mataifa mbalimbali imeathiri pakubwa biashara.